Injue Vita vya Afghanistan na Talibani ni kundi la aina Gani?
Kingmaja_Tv Vita vya Afghanistan: Je, Taliban ni kundi la aina gani ? 16 Agosti 2021 Wapiganaji wa kundi la Taliban CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Kundi la Taliban liliondolewa madarakani nchini Afghanistan na vikosi vilivyoongozwa na Marekani mwaka 2001 lakini taratibu kundi hilo likaanza kujiimarisha tangu wakati huo na sasa hivi limeiteka upya Afghanistan Lakini je Taliban ni kina nani? Taliban lina maanisha wanafunzi katika lugha ya Kipashto na lilianza kuchipuka mapema miaka ya 1990 kaskazini mwa Pakistan kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Umoja wa Usovieti nchini Afghanistan. Je! Taliban ina nguvu gani za kuweza kulishinda jeshi la serikali? Mfahamu Haibatullah, Kiongozi mtata wa Taliban mwenye jina la kike Inaaminika kwamba vuguvugu la Pushtun kwanza lilianza kujitokeza katika mikutano ya kidini ambayo mara nyingi ilikuwa inasimamiwa kifedha na Saudi Arabia - ambalo lilikuwa linahubiri msimamo mkali wa Waislamu wa Sunni. Ahadi iliyotolewa na Taliban - katika maeneo ya Pashtun zil